Apr 10, 2024 03:04 UTC
  • Mzozo kati ya Ethiopia na Somalia wazidi kuongezeka

Tangu kutangazwa kwa makubaliano ya bahari kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland miezi mitatu iliyopita, hali ya mvutano imekuwa ukiendelea kati ya nchi hizo mbili jirani za mashariki mwa Afrika na washirika wa usalama.

Tarehe 4 mwezi huu Somalia ilimwamuru balozi wa Ethiopia kuondoka nchini humo katika muda wa saa 72 na kufungwa balozi zake ndogo katika maeneo yalilojitenga ya Somaliland na Puntland.  

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia ilieleza kuwa wanadiplomasia na wafanyakazi wa balozi hizo wanapaswa kuondoke Somalia ndani ya wiki moja. Somalia pia ilimwita nyumbani balozi wake nchini Ethiopia kwa ajili mashauriano. 

Mwezi Januari mwaka huu Ethiopia ilisaini hati ya maelewano na Somaliland; ambapo Somalia ilipinga makubaliano hayo ikisema yanakiuka mamlaka yake na umoja wa ardhi ya nchi hiyo. Makubaliano hayo yangeiruhusu Ethiopia kutumia bahari kupitia Somaliland; na mkabala wake, Ethiopia ingeitambua rasmi Somalinad kama nchi huru. 

Azimio la Baraza la Mawaziri la Somalia lilitaja uingiliaji wa Ethiopia katika "mambo ya ndani" ya Somalia kama sababu ya maamuzi hayo.

Tags