Apr 28, 2024 07:19 UTC
  • Wapiganaji 70 wa kundi la kigaidi la al-Shabab waangamizwa Somalia

Kwa akali wapiganaji 70 wa kundi la kigaidi la al-Shabab wameangamizwa nchini Somaliia kufuatia operesheni ya jeshi dhidi yao.

Ripoti zinaeleza kuwa, jeshi la Somalia limefanikiwa kuwaua wanachama 70 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini humo na kujeruhi idadi nyingine ya magaidi hao wakati wa operesheni ya kipekee.

Kwa mujibu wa taarifa, jeshi la Somalia lilitangaza kuwa katika operesheni katika msitu wa Tabar Mooge katikati mwa nchi hiyo, limefanikiwa kuwaua wanachama 70 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab.

Kulingana na ripoti, magaidi wa al-Shabaab walikuwa wamekusanyika katika vituo 3 vya kijeshi vilivyoko katika eneo hilo, na kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, idadi yao imefikia magaidi 150 wenye silaha.

Jeshi la Somalia limesisitiza kuwa, wanajeshi wa jeshi la nchi hiyo wanawasaka magaidi waliokimbilia katika misitu ya eneo hilo baada ya operesheni hiyo.

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la al-Shabab

 

Hivi majuzi Wizara ya Ulinzi ya Somalia ilitangaza habari ya kuangamizwa magaidi tisa wa al-Shabaab katika eneo la Bay la kusini mwa nchi hiyo ya eneo la Pembe ya Afrika.

Tangu mwaka 2007, magaidi wa al-Shabaab wamekuwa wakipigana na serikali ya Somalia na Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini humo (ATMIS) lakini mashambulizi yake yamekuwa ya kifeli hasa baada ya genge hilo kufurushwa kwenye miji mikubwa ya Somalia na kubakia katika baadhi ya vijiji ambako inavitumia kuendesha mashambulizi ya kuvizia na ya chini kwa chini.

Kikosi cha ATMIS cha Umoja wa Afrika kimetumwa huko Somalia kwa baraka kamili za  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.