May 05, 2024 04:16 UTC
  • Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu unafanyika Gambia

Mkutano wa 15 wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ulianza jana Jumamosi katika mji mkuu wa Gambia, Banjul.

Viongozi wa dunia kutoka nchi 57 wanachama wa OIC na kwingineko wanahuhudhuria mkutano huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya sektretarieti ya OIC, mkutano huo unalenga kuimarisha umoja "katika kushughulikia kwa pamoja changamoto kubwa zinazoukabili Ummah wa Kiislamu na kupanua ushirikiano na mshikamano kati ya nchi wanachama katika kutekeleza malengo ya pamoja kama yalivyoainishwa katika hati ya jumuiya."

OIC iliongeza kuwa mkutano huo pia unalenga "kupanua uchumi wa ndani na kufufua biashara ndogo na za kati," pamoja na "kuchukua fursa ya kutambulishai wa utamaduni wa Gambia na Afrika."

Mkutano huo ulioanza Jumamosi unamalizika leo Jumapili pia unashughulikia masuala ya kimataifa, hususan hali ya sasa ya Palestina na vita vinavyoendelea vya Israel katika Ukanda wa Gaza ambavyo vimepelekea Wapalestina karibu 35,000 kupoteza maisha, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.

Gambia itachukua uenyekiti wa mkutano huo kutoka Saudi Arabia na itakuwa mwenyekiti wa OIC kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.