Kagame: Sijawahi kuweka masharti ya kukutana na Félix Tshisekedi
Rais Paul Kagame wa Rwanda amezungumzia uhusiano uliopo kati ya nchi yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambao umezorota katika siku za hivi karibuni kutokana na kuongezeka mivutano.
Rais Kagame ameeleza kuwa, siku zote amekuwa yuko tayari kukutana na mwenzake wa DRC kwa ajili ya mazungumzo na kwamba, hakuna wakati ambao aliweka masharti.
Rais Kagame amemkosoa Rais Felix Tshisekedi na kubainisha kwamba, kwangu mimi, ndiye anayeweka masharti. Sijawahi kuweka masharti kabla ya kukutana naye. "
Alipoulizwa kufanikiwa kwa upatanishi wa Angola kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Paul Kagame amemshambulia mwenzake wa Kongo Félix Tshisekedi.
Kwa jinsi tunavyohusika, Rwanda, tumekuwa wazi sana," amesema: "Siku zote tumekuwepo, tumechangia kila tuwezavyo kufanya kazi hii yote. Lakini inaonekana kuwa DRC ina mawazo mengine.
Rais wa Angola ambaye anahudumu kama msuluhishi aliyeteuliwa na Umoja wa Afrika (AU) amekuwa akifanya juhudi za kuwakutanisha viongozi hao wawili ingawa tarehe mahsusi ya kukutana ana kwa ana haijatangazwa hadi sasa.
Rais Felix Tshisekedi alisema hivi karibuni kwamba, yuko tayari kusitisha mpango wake wa kuanzisha vita na jirani yake Rwanda, ili kutoa nafasi kwa jitihada zinazoendelea za kupata suluhu ya mzozo unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikimtuhumu jirani yake Rwanda kuwa inaliunga mkono kundi la waasi wa M23, madai ambayo yanakanushwa na Kigali, lakini yanaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.