Jeshi la Nigeria laangamiza magaidi 2,245 ndani ya miezi 3
(last modified Sat, 29 Jun 2024 12:19:50 GMT )
Jun 29, 2024 12:19 UTC
  • Jeshi la Nigeria laangamiza magaidi 2,245 ndani ya miezi 3

Mkurugenzi wa shughuli za vyombo vya habari vya jeshi la Nigeria, Meja Jenerali Edward Buba amesema kuwa watu 1,993 waliokuwa wametekwa nyara wameokolewa baada ya wahalifu kupewa kikomboleo huku, silaha 2,783 za magaidi zikinaswa.

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaangamiza magaidi 2,245 katika oparesheni dhidi ya wanamgambo wa kitakfiri wa Boko Haram na wale wa kundi la ISWAP miezi mitatu iliyopita. ISWAP ni tawi la magaidi wa Deash (ISIS) huko Magharibi mwa Afrika. 

Meja Jenerali Buba amesema kuwa, oparesheni hizo zimetekelezwa dhidi ya makundi ya kigaidi katika majimbo tofauti ya Nigeria kuanzia Aprili hadi mwezi huu wa Juni. 

Nigeria hivi karibuni ilikumbwa na mashambulizi ya magenge ya uhalifu yakiwemo makundi ya magaidi wa Boko Haram na ISWAP katika majimbo mbalimbali ya nchi hiyo. Makundi hayo ya kigaidi yamekuwa yakiwateka nyara watu nchini Nigeria mkabala wa kupatiwa fedha kama kikomboleo licha ya kuainishwa hukumu ya kifo kwa vitendo vya utekaji nyara nchini Nigeria.

Makundi ya wanamgambo wenye silaha 

Makundi yenye silaha kwa kawaida hushambulia vijiji, shule na wasafiri katika maeneo ya kaskazini mwa Nigeria na baadaye  kudai kikomboleo.