Mkutano kuhusu uhusiano na utawala haramu wa Israel waahirishwa nchini Morocco
Mkutano uliopangwa na utawala dhalimu wa Israel kuhusu uhusiano wa kawaida na Morocco umeakhirishwa katika nchi hiyo ya kasakzini mwa Afrika kutokana na hofu ya kuibuuka maandamano ya wananchi.
Shirika la Habari la Quds linaripoti kuwa, uutawala ghasibu wa Israel umeripotiwa kuakhirisha mkutano huo.
Mkutano huo ulipangwa kufanyika huko Casablanca Morocco kwa ushiriki wa wasomi wa Kiyahudi na Kiislamu.
Spika wa bunge la Morocco pia alipangwa kulihutubia mkutano huo.
Waandaaji wameahirisha mkutano huo kwa hofu kwamba watu waliochukizwa na vita vya mauaji ya halaiki vya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza watafanya maandamano makubwa.
Mkutano huo umeakhirishwa mara mbili hapo kabla ambapo, mara ya kwanza mwezi Mei, 2024 na mara nyingine mwezi Juni, 2024.
Bado hakuna tarehe mpya iliyotangazwa kwa ajili ya kuufanyika mkutano huo.
Maelfu ya wananchi wa Morocco wamekuwa wakifanya maandamano ya mara kwa mara katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani jinai zinazoendelea kufanywa na jeshi la Israel huko Gaza. Kadhalika wananchi wa Moroco wanaishinikiza pia serikali ya Rabat kufuta makubaliano ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala katili wa Israel.
Desemba 2020, Morocco na utawala haramu wa Israel zilifikia mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida kwa ushawishi wa Marekani. Na kama sehemu ya makubaliano hayo, Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump alikubali kutambua mamlaka ya Morocco juu ya Sahara Magharibi.