Kagame ashambulia ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyolaani serikali ya Kigali
-
Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame amekosoa ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akisema kwamba iliandikwa na "wataalamu ambao wanasimulia hadithi kwa njia inayoonyesha kwamba hawana uzoefu katika faili hilo.
Kagame aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigali ameongeza kwamba wataalamu hawa "wanazungumza juu ya uwepo wa vikosi vya Rwanda mashariki mwa Congo DR na kupuuza kabisa uwepo wa vikosi vya wapinzani wenye silaha wanaojulikana kama Democratic Forces for the Liberation of Rwanda, na ushirikiano wao na jeshi la Congo."
Rais wa Rwanda amedokeza kwamba mjadala kuhusu tatizo la sasa Mashariki mwa Congo unapaswa uwe katika muktadha wa matatizo yanayoikabili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwani “Congo ya mashariki ni sehemu muhimu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na si nchi nyingine inayojitegemea.”
Kagame amehusisha machafuko ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na enzi za ukoloni, na kusema kuwa nchi za kikoloni zilitawanya baadhi ya makabila katika zaidi ya sehemu moja.
Akiashiria raia wa Congo DR wenye asili ya Kitutsi, Rais Kagame amesema kuwa serikali ya Kinshasa inakubali kwamba wao ni raia, lakini inaendelea kuunga mkono makundi ya waasi wenye silaha, hasa Democratic Forces for the Liberation of Rwanda, ambayo yanakumbatia itikadi ya mauaji ya kikabila na kutoa msaada wa fedha na silaha kwa makundi hayo.

Kagame amesema kuwa nchi yake ina taarifa za kuwepo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo watu wasiopungua 20 waliopanga, kuunga mkono na kueneza itikadi ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, na kwamba wanafanya kazi ya kudumisha itikadi za mauaji ya halaiki, ambayo bado yanatishia eneo hilo.”
Siku chache ziliziopita Umoja wa Mataifa ufichua katika ripoti yake kuwa, kati ya wanajeshi 3,000 hadi 4,000 wa Rwanda wanapigana bega kwa bega na waasi wa kundi la M23 huko mashariki mwa Congo DR, huku Kigali ikiongoza pakubwa oparesheni za kundi hilo.