Gen Z waandamana tena leo nchini Kenya kumshinikiza Ruto ajiuzulu
Maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z nchini Kenya ambayo katika siku za hivi kariibuni yameitikisa serikali ya Rais William Ruto yamefanyika leo pia katika baadhi ya miiji mikubwa ya nchi hiyo.
Baadhii ya miji ya Kenya kama mji mkuu Nairobi na Mombasa imeshuhudia maandamano hayo huku vijana wakiwa wamebeba mabango yenye maandishi ya kumtaka Rais William Ruto ajiuzulu.
Jiji Nairobi polisi ililazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawala waandamanaji.
Wafanyabiashara mjini Nairobi hawakufungua maduka yao leo wakihofia uharibifu ambao umekuwa ukifanywa dhidiiya mali na waandamanaji huku baranara nyingi za jiji hilo zikifungwa.
Rais William Ruto jana aliujia juu Wakfu wa Ford wa Marekani, akiuhusisha na vurugu zilizoshuhudiwa nchini humo wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024 na jinsi utawala wa Kenya Kwanza unaendesha serikali.
Maandamano yaliyosukumwa na vijana wa kizazi cha Gen Z yalitikisa nchi hiyo ya Afrika Mashariki Juni 25, na kuishia kusababisha vifo vya watu 42 huku waandamanaji wengine wakitekwa nyara.
Wakati huo huo, viongozi wa kidini nchini Kenya, wakiongozwa na Baraza la Maimamu na Wahubiri nchini humo (CIPK) wamewataka vijana nchini Kenya kusitisha maandamano yao yanayotarajiwa kuendelea leo Jumanne, wakihofia kudorora kwa usalama.
CIPK inasema licha ya kuwa maandamano ni haki ya kikatiba, wanaoshiriki wanapaswa kuwa waangalifu kuhakikisha amani inadumishwa.