Pande hasimu za Sudan zakutana Geneva kujadili mgogoro wa kibinadamu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i114232-pande_hasimu_za_sudan_zakutana_geneva_kujadili_mgogoro_wa_kibinadamu
Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yalianza Julai 11 nchini Uswisi kati ya wajumbe kutoka kwa pande mbili hasimu nchini Sudan, chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, ili kujaribu kufikia uusitishaji mapigano na kuruhusu kuwafikia watu walio hatarini.
(last modified 2024-07-19T03:54:11+00:00 )
Jul 19, 2024 03:54 UTC
  • Pande hasimu za Sudan zakutana Geneva kujadili mgogoro wa kibinadamu

Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yalianza Julai 11 nchini Uswisi kati ya wajumbe kutoka kwa pande mbili hasimu nchini Sudan, chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, ili kujaribu kufikia uusitishaji mapigano na kuruhusu kuwafikia watu walio hatarini.

Mgogoro nchini Sudan ndio mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani, unasema Umoja wa Mataifa, huku zaidi ya Wasudan milioni 13 wakiwa wamehama au kuwa wakimbizi.

Aidha kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, nusu ya idadi ya watu  wanakabiliwa na uhaba wa chakula. Wakati nchi hiyo ikitumbukia katika "moja ya majanga mabaya zaidi" kulingana na Umoja wa Mataifa, idadi kubwa ya shughuli za kibinadamu zimekatizwa kutokana na ukosefu wa usalama.

Daktari Shible Sabhani, mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Sudan anasema kuwa, hali ni mbaya hasa katika mji mkuu Khartoum, katika mikoa ya Kordofan, Al-Jazirah na hasa Darfur.

Vita vilizuka mwezi Aprili mwaka 2023 kati ya jeshi la serikali na kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF), na kuitumbukiza Sudan katika “moja ya mizozo mibaya ya kibinadamu katika kumbukumbu za hivi karibuni”, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Majenerali hasimu wa Sudan ambao wameitumbikiza nchi yao katika vita vya wenyewe kkwa wenyewe

 

Asasi mbalimbali za kieneo na kimataifa zimekuwa zikitahadharisha kuhusiana na kuzidi kuzorota hali ya kibinadamu nchini Sudan.

Sudan ilitumbulia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu Aprili 15, 2023 kati ya jeshi la nchi hiyo linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) chini ya amri ya Mohammed Hamdan Dagalo.