Uganda wasisitiza kuandama licha la onyo kali la Rais Museveni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i114344-uganda_wasisitiza_kuandama_licha_la_onyo_kali_la_rais_museveni
Waandamanaji nchini Uganda wametangaza kuwa, wataendelea na mipango yao ya kufanya mkusanyiko mnamo Jumanne ijayo licha ya marufuku na serikali.
(last modified 2024-07-22T03:47:02+00:00 )
Jul 22, 2024 03:47 UTC
  • Uganda wasisitiza kuandama licha la onyo kali la Rais Museveni

Waandamanaji nchini Uganda wametangaza kuwa, wataendelea na mipango yao ya kufanya mkusanyiko mnamo Jumanne ijayo licha ya marufuku na serikali.

Sisitizo hilo wanalitoa katika hali ambayo, Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni ametoa onyo kali dhidi ya hatua hiyo na kuwaambia "wanacheza na moto", kwa mipango yao ya kufanya maandamano makubwa.

Rais Museveni amesisitiza kuwa, kuna baadhi ya makundi yamekuwa yakipanga kufanya maandamano batili na vurugu.

Rais Museveni ambaye anaitawala Uganda tangu alipoingia madarakani mwaka 1986 amesema kuwa, kuna ishara za waandamanaji kuwa na malengo ya kile ambacho amekitaja kuwa "kutimiza maslahi ya kigeni". Hata hivyo Museveni ambaye anatuhumiwa kutawala kwa mkono wa chuma hakufafanua zaidi kuhusiana na kauli yake hiyo.

Frank Mwesigwa, Mkuu wa operesheni za polisi ya Uganda

 

Mapema siku ya Jumamosi, polisi ya Uganda iliwaarifu wale wanaopanga kufanya maandamano hayo kwamba haitayaruhusu. Taarifa hiyo ilisema kwamba, vyombo vya usalama vimepata taarifa za kiintelejinsia zinazobainisha kwamba, kuna ishara ya makundi yanayotaka kutumia maandamano hayo yalipangwa kwenye mji mkuu Kampala "kuzusha machafuko nchini humo".

Mkuu wa operesheni za polisi ya Uganda Frank Mwesigwa amesema kuwa, maandamano yanapaswa kuandaliwa chini ya ruhusa yetu kwa msingi kwamba hakuna vurugu itakayotokea au kuvuruga maisjh ya raia wengine.

Hata hivyo wale waliopanga maandamano wameapa kuendelea nayo licha ya zuio hilo la polisi. "Hatuhitaji kibali cha polisi kufanya maandamano ya amani," amesema mmoja ya viongozi wa maandamano hayo, Louez Aloikin akisisitiza kuwa, “ni haki yetu ya kikatiba".