Algeria yamwita nyumbani balozi wake kulalamikia hatua ya Ufaransa kuhusu Sahara Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i114672-algeria_yamwita_nyumbani_balozi_wake_kulalamikia_hatua_ya_ufaransa_kuhusu_sahara_magharibi
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Algeria imemwita nyumbani balozi wake kutoka Ufaransa kupinga hatua ya serikali ya Paris kuingilia kati mpango wa Sahara Magharibi wa kuwa na mamlaka ya ndani.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Jul 31, 2024 03:56 UTC
  • Algeria yamwita nyumbani balozi wake kulalamikia hatua ya Ufaransa kuhusu Sahara Magharibi

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Algeria imemwita nyumbani balozi wake kutoka Ufaransa kupinga hatua ya serikali ya Paris kuingilia kati mpango wa Sahara Magharibi wa kuwa na mamlaka ya ndani.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Algeria imeeleza kuwa, Algeria imeamua kumuita nyumbani mara balozi wake kutoka Paris baada ya Ufaransa kutangaza kuunga mkono mpango wa Sahara Magharibi wa kuwa na Mamlaka ya Ndani.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza kuwa, serikali ya Ufaransa imetangaza uungaji mkono wake wa moja kwa moja na wa wazi kwa jambo lililowekwa na kutwishwa na ukoloni katika eneo la Sahara Magharibi; hakuna hata serikali moja zilizotanguulia nchini Ufaransa iliyofanya jambo kama hilo, lakini serikali ya sasa imechukua uamuzi huu usio na tadibiri na bila kuzingatia matokeo yake.

Morocco ililitwaa eneo kubwa la Sahara Magharibi, koloni la zamani la Uhispania mwaka 1975 na tangu wakati huo imekuwa katika mzozo na mapigano na Harakati ya Polisario, inayoungwa mkono na Algeria, ambayo inapigania kuasisi nchi huru katika eneo hilo na kukomesha uwepo wa serikali ya Rabat.

Harakati ya Polisario inaungwa mkono na Algeria.

 

Kwa sasa, Morocco inadhibitii asilimia 80 ya eneo la Sahara Magharibi huku sehemu iliyosalia ikishikiliwa na Harakati ya Polisario inayoungwa mkono na Algeria. Kwa zaidi ya miaka 15, Polisario imepigana vita na Morocco vya kulikomboa eneo hilo, baada ya Uhispania kuondoa askari wake mwaka 1975 na inataka iitishwe kura ya maoni ya kuamua uhuru na kujitawala watu wa Sahara Magharibi

Uamuzi wa Algeria wa kumrejesha nyumbani balozi wake wa Paris ni ishara ya kuharibika uhusiano wa kidiplomasia baina ya Algiers na Paris.