Jeshi la Sudan lazima shambulio la wanamgambo wa RSF
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i114850-jeshi_la_sudan_lazima_shambulio_la_wanamgambo_wa_rsf
Jeshi la Sudan limeripoti kwamba limefanikiwa kuzima shambulio la wanamgambo wa RSF dhidi ya Jimbo la Blue Nile kusini mashariki mwa Sudan. Jeshi limesema vikosi vyake vimezuia shambulio hilo katika eneo la Guli.
(last modified 2024-08-05T01:23:47+00:00 )
Aug 05, 2024 01:23 UTC
  • Jeshi la Sudan lazima shambulio la wanamgambo wa RSF

Jeshi la Sudan limeripoti kwamba limefanikiwa kuzima shambulio la wanamgambo wa RSF dhidi ya Jimbo la Blue Nile kusini mashariki mwa Sudan. Jeshi limesema vikosi vyake vimezuia shambulio hilo katika eneo la Guli.

Iimeongeza kuwa limekamata vifaa vya RSF na kuwazuia makumi ya wapiganaji wa RSF.katika Jimbo la Blue Nile pamoja na majimbo 13 kati ya 18 nchini Sudan ambayo yameathiriwa moja kwa moja na ghasia zinazoendelea.

Vita nchini Sudan vilizuka mwezi Aprili 2023 kati ya Jenerali wa Jeshi Abdel Fattah al-Burhan na kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo baada ya kutoelewana kuhusu kuingizwa RSF katika jeshi.

Mzozo huo umesababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu ambapo mapigano yameua karibu watu 16,000 na kalazimisha mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.

Sudan iliwasilisha malalamiko kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo Machi 29 dhidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu kwa madai ya kuunga mkono RSF, madai ambayo UAE imeyakanusha.