Hatimaye wanajeshi wa mwisho wa Marekani waondoka Niger
Hatimaye wanajeshi wa mwisho wa Marekani wameondoka nchini Niger, zaidi ya mwaka mmoja baada ya viongozi wa mapinduzi kuwataka kuondoka.
Baada ya wanajeshi 800 kuondoka kambini katika mji mkuu wa Niamey mapema mwezi Julai, takriban wanajeshi 200 walibaki katika kambi kubwa ya Agadez kaskazini mwa Niger.
Mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wa Marekani na vifaa vyao katika uwanja wa kijeshi huko Agadez umekamilika,” wizara ya ulinzi wa Marekani (Pentagon) ilisema katika taarifa ya pamoja na wizara ya ulinzi wa Niger.
Naibu msemaji wa wizara ya ulinzi Sabrina Singh aliwaambia waandishi wa habari kwamba “chini ya wanajeshi 20” bado wako uwanjani nchini Niger.
Alisema waliobaki wapo kwenye ubalozi wa Marekani na wanaendelea na shughuli za utawala wakijiandaa kwa ajili ya kukamilisha zoezi la kuondoka.”
Kambi ya mwisho ya kijeshi ya Marekani nchini Niger ilikabidhiwa juzi Jumatatu kwa nchi hiyo ya Kiafrika huku nchi tatu za Niger, Mali na Burkina Faso zikipanga kuunda kikosi cha pamoja cha kuwatimua wanajeshi wa kigeni, wakiwemo wa Marekani.
Mwezi uliopita, wanajeshi wa Marekani waliondoka kwenye kambi ndogo ya ndege zisizo na rubani ya 101 iliyoko katika mji mkuu wa Niger, Niamey.
Serikali mpya ya Niger imewatimua wanajeshi wa Marekani baada ya kupinduliwa Rais wa Niger aliyekuwa kibaraka mkubwa wa nchi za Magharibi mwezi Julai mwaka jana. anajeshi wa Ujerumani pia wamepangiwa kuondoka nchini Niger ifikapo tareje 31 ya mwezi huu.