Botswana yatangaza mapumziko kusherehekea medali ya dhahabu katika michezo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i115036-botswana_yatangaza_mapumziko_kusherehekea_medali_ya_dhahabu_katika_michezo
Rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana jana alitangaza Ijumaa alasiri kuwa sikukuu ya kusherehekea ushindi wa Letsile Tebogo, ambaye siku ya Alhamisi aliandika historia ya kutwaa medali ya kwanza ya dhahabu kwa nchi hiyo katikak mbio hizo.
(last modified 2024-08-09T23:01:58+00:00 )
Aug 09, 2024 23:01 UTC
  • Botswana yatangaza mapumziko kusherehekea medali ya dhahabu katika michezo

Rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana jana alitangaza Ijumaa alasiri kuwa sikukuu ya kusherehekea ushindi wa Letsile Tebogo, ambaye siku ya Alhamisi aliandika historia ya kutwaa medali ya kwanza ya dhahabu kwa nchi hiyo katikak mbio hizo.

Mwanariadha huyo ameingia katika kumbukumbu za historia kwa kuwa Mwafrika wa kwanza kushinda mbio za Olimpiki za mita 200, mashindano ambayo yanaendelea huko Paris Ufaransa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 aliwapita wapinzani wake Kenny Bednarek na Noah Lyles mjini Paris na kushinda medali ya kwanza ya dhahabu ya Olimpiki ya Botswana katika mchezo wowote.

Akitangaza mapuumziko ya nusu siku kusherehekea ushindi huo, Rais wa Botswana alisema kuwa, mafanikio ya Tebogo "yataandikwa katika kumbukumbu za historia ya nchi".

 

Makamu wa rais wa Kamati ya Taifa ya Olimpiki ya Botswana, Tshepo Sitale ameziambia duru za habari kwamba kamati hiyo "ilikuwa na furaha isiyo na kifani" kufuatia mafanikio ya mwanariadha huyo.

Tebogo sasa anatambuliwa kama mtu wa tano kwa kasi zaidi katika historia kwa umbali. Ametunuku ushindi wake kwa marehemu mama yake, ambaye aliaga dunia mwezi Mei.