Oct 01, 2024 06:21 UTC
  • Burkina Faso: Madola ajinabi yanawazidishia matatizo kwa makusudi  watu wa Sahel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso jana alihutubia katika majadiliano ya ngazi ya juu katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York na kusema nchi yake inaendelea kupambana na makundi ya kigaidi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo yanayoyumbisha hali ya usalama nchini humo.

Karamoko Jean Marie Traore amesema kuwa muungano wa nchi za Sahel kimsingi ulikusudiwa kwa madhumuni ya kuwalinda raia wa nchi za eneo hilo ambao wametaabika kwa ukosefu wa amani na uthabiti. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso kwa mara nyingine tena ameituhumu Ukraine kuwa inafadhili magaidi katika eneo la Sahel. "Muungano wa Sahel umeasisiwa lengo lake kuu likiwa ni kulinda wakazi wa nchi za eneo hilo ambao wameteseka na kutaabika na hali ya ukosefu wa amani iliyosababishwa na makundi ya kigaidi", amesema Karamoko Marie Traore.  

Ameongeza kuwa, Burkina Faso inaunga mkono kufanyika marekebisho katika Baraza la Usalama la UN ambayo yatalijumuisha pia bara la Afrika. 

 

Tags