Oct 09, 2024 07:03 UTC
  • Watu 21 wafariki dunia baada ya boti kugongana nchini Nigeria

Polisi ya Nigeria jana ilithibitisha kupoteza maisha takriban watu 21 baada ya boti mbili za abiria ambazo hazikuwa zimesajiliwa kupinduka. Boti hizo zilipinduka baada ya kugongana katika jimbo la Lagos nchini Nigeria.

Ajali hiyo ya boti ilitokea katika mji wa Imore katika eneo la Amuwo-Odofin katika jimbo la Lagos. 

Boti hizo mbili ambazo kila moja ilikuwa imebebea abiria 16 zilipinduka zikiwa katikati ya ziwa.

Benjamin Hundeyin Msemaji wa Polisi katika jimbo la Lagos ameeleza kuwa abiria 11 waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali ya jeshi la majini huko Alakija.

Ameongeza kuwa idara ya uokoaji inaendelea kusaka miili ya wahanga waliozama majini na kwamba tayari uchunguzi umeanza kuhusu chanco cha ajali hiyo ya boti. 

Wiki jana watu 48 walipoteza maisha na wengine wasiopungua 150 walizama majini baada ya boti kupinduka na kuzama katika jimbo la Kebbi huko Nigeria.

Boti hiyo ilikuwa na abiria wasiopungua 300.

 

Tags