Al-Burhan: Vita vinakaribia kuisha na hakuna mapatano na maadui wa taifa
(last modified Wed, 20 Nov 2024 08:07:28 GMT )
Nov 20, 2024 08:07 UTC
  • Al-Burhan: Vita vinakaribia kuisha na hakuna mapatano na maadui wa taifa

Mkuu wa Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan, amesema wakati wa mkutano wa kiuchumi katika mji wa Port Sudan kwenye pwani ya Bahari Nyekundu kwamba vita na kundi la RSF inakaribia mwisho, ikisisitiza kwamba hakuna nafasi ya mazungumzo na mapatano na kile alichokiita “maadui wa taifa.”

Al Burhan ambayye ni kamanda wa jeshi al Sudan amesema: "Vita hii iko mwisho mwake. Hakuna fursa ya kufanya amani na maadui wa taifa la Sudan na tunapinga uingiliaji wa mataifa ya kigeni na amri zao kwa Sudan."

Abdel Fattah Al-Burhan amesisitiza kuwa, kundi la Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na wafuasi wake hawana nafasi yoyote katika mustakbali wa Sudan.

Kiongozi wa Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan amesema Sudan haikukubaliana na rasimu ya azimio la Uingereza, kama baadhi ya watu walivyodai na kwamba rasimu ya azimio la Uingereza inakiuka mamlaka ya Sudan.

Hivi majuzi Uingereza iliwasilisha rasimu ya azimio katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikitaka kusitishwa mara moja kwa uhasama nchini Sudan na kulindwa raia kutokana na vita vya ndani ambavyo vimeisambaratisha nchi hiyo tangu Aprili 2023.