Ouattara: Ufaransa kuondoa wanajeshi wake Ivory Coast
(last modified Wed, 01 Jan 2025 13:05:05 GMT )
Jan 01, 2025 13:05 UTC
  •  Alassane Ouattara
    Alassane Ouattara

Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast amesema kuwa wanajeshi wa Ufaransa wataondoka nchini humo mwezi huu wa Januari. Rais wa Ivory Coast alieleza haya jana Jumnanne katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka kwa taifa.

Rais wa Ivory Coast amesema kuwa nchi hiyo sasa inaweza kujivunia jeshi lake ambalo limeboreka na ni kwa muktadha huu wameamua kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa nchini humo. Ouattara amesema, kambi ya Kikosi cha 43 cha Wanamaji huko Port Bouet itarejeshwa kwa wanajeshi wa nchi hiyo.

Hatua hii ya Ivory Coast inafuatia uamuzi sawa uliochukuliwa na Mali, Burkina Faso na Niger. 

Serikali ya Chad ilitangaza tarehe 28 Novemba kwamba, imefuta makubaliano yake ya kijeshi na serikali ya Ufaransa kuhusu uwepo wa wanajeshi 1,000 wa Ufaransa nchini humo.

Wanajeshi wa Ufaransa wakiondoka Chad 

Ufaransa ilikoloni nchi ishirini za Kiafrika kwa miongo kadhaa. Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia na wimbi la uhuru wa makoloni ya wakoloni wa Ulaya, mkoloni huyu wa Ulaya alijaribu kudumisha ushawishi wake barani Afrika na uwepo wa kijeshi katika baadhi ya makoloni yake ya zamani.

Ingawa Ufaransa inajiona kuwa chimbuko la demokrasia, lakini ilifanya njama za  kudumisha satwa yake ya kijeshi na kiuchumi barani Afrika kwa kuunga mkono serikali za kidiktteta ambazo ni makoloni yake ya zamani.