Wafadhili waahidi dola bilioni 8 kusambaza umeme Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i122074-wafadhili_waahidi_dola_bilioni_8_kusambaza_umeme_afrika
Benki ya Maendeleo ya Afrika na wakopeshaji wengine wa kimataifa wameahidi zaidi ya dola bilioni 8 zitakazotumika kwenye mkakati wa kuwawezesha Waafrika milioni 300 kupata umeme katika kipindi cha miaka sita ijayo. Mpango huo unaoitwa "Mission 300" uliozinduliwa na Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika mwezi Aprili, unakadiriwa kugharimu dola bilioni 90.
(last modified 2025-01-29T22:27:03+00:00 )
Jan 29, 2025 22:27 UTC
  • Wafadhili waahidi dola bilioni 8 kusambaza umeme Afrika

Benki ya Maendeleo ya Afrika na wakopeshaji wengine wa kimataifa wameahidi zaidi ya dola bilioni 8 zitakazotumika kwenye mkakati wa kuwawezesha Waafrika milioni 300 kupata umeme katika kipindi cha miaka sita ijayo. Mpango huo unaoitwa "Mission 300" uliozinduliwa na Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika mwezi Aprili, unakadiriwa kugharimu dola bilioni 90.

Utekelezwaji wake hata hivyo unakabiliwa na changamoto kutokana na uchumi dhaifu wa mataifa ya Afrika, hasa kutokana na makusanyo duni ya mapato na gharama kubwa za mikopo.

Viongozi kwenye Mkutano wa kilele wa Nishati barani Afrika uliofanyika Dar es Salaam, Tanzania wamesema nusu ya walengwa hao wataunganishiwa umeme wa gridi za taifa zilizopo, na nusu nyingine itatokana na vyanzo vya nishati mbadala, ikijumuisha gridi ndogo za upepo na jua.

Viongozi wa nchi za Afrika walioshiriki mkutano wa Dar es Salaam wameazimia kutengeneza mazingira bora ya kisera ya kisheria ili kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya nishati.

Marais na wakuu wa nchi za Afrika wamekubaliana kuhakikisha wanawekeza zaidi na kushirikiana katika miradi ya pamoja na umeme ili kufikia lengo la kuwafikishia nishati hiyo wananchi milioni 300 ifikapo 2030.

wameazimia kukubaliana kwamba karibu Waafrika milioni 600 hawajafikiwa na huduma ya umeme, na bilioni moja hawatumii nishati safi ya kupikia, licha ya hatua zilizopigwa.