Jeshi la Sudan latangaza kudhibiti maeneo mengi ya mashariki mwa Khartoum
Ripoti kutoka Sudan zinasema, jeshi la nchi hiyo linakaribia kutangaza mji wa Khartoum Bahri kuwa huru kutoka kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) baada ya kuchukua udhibiti wa vitongoji vyote vya jiji hilo.
Jeshi la Sudan limetangaza kuwa limeudhibiti kikamilifu mji wa Khartoum Bahri, mojawapo ya maeneo makuu matatu ya mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
Taarifa ya jeshi la Sudan imesema, kwamba vikosi vyake vimedhibiti mhimili wa Al-Mak Bridge, kusini mwa Khartoum Bahri, na kwamba vinasonga mbele kusafisha eneo hilo.
Majukwaa ya kijamii jeshi la Sudan yamerusha hewani video zinazoonyesha wanajeshi wakiingia katika vitongoji vya kusini na magharibi vya Khartoum Bahri, na upande wa kaskazini wa Daraja la Mak Nimr, ambalo linaelekea katikati mwa mji mkuu na ikulu ya rais, inayodhibitiwa na wapiganaji wa RSF.
Khartoum Bahri ni moja ya miji mitatu inayounda mji mkuu wa Sudan, pamoja na Omdurman na Khartoum.
Hapo awali jeshi la Sudan lilikuwa limedhibiti maeneo makubwa ya Omdurman.