Takriban watu 70 wauawa katika mapigano ya Puntland, Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i122412-takriban_watu_70_wauawa_katika_mapigano_ya_puntland_somalia
Takribani watu 70 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia mapigano ya saa 24 kati ya wapiganaji wa Islamic State na vikosi vya eneo la Somalia la Puntland.
(last modified 2025-02-06T23:11:37+00:00 )
Feb 06, 2025 23:11 UTC
  • Takriban watu 70 wauawa katika mapigano ya Puntland, Somalia

Takribani watu 70 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia mapigano ya saa 24 kati ya wapiganaji wa Islamic State na vikosi vya eneo la Somalia la Puntland.

Takriban wanajeshi 15 wa Puntland na zaidi ya wanamgambo 50 walikufa kwenye mapigano hayo kwenye maeneo ya Dharin na Qurac kwenye milima ya Cal Miskaad huko Bari Puntland.

Taarifa hizo zimetolewa na maafisa kadhaa wa usalama wa Puntland walipozungumza na duru za habari kwa sharti ya kutotajwa kwa kuwa hawajaruhusiwa kuongea na vyombo vya habari.

Msemaji wa operesheni ya usalama wa Puntland Brigedia Jenerali Mohamud Ahmed ameziambia duru za habari kwamba, mapigano hayo yaliyoanza siku ya Jumanne yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kkushuhudiwa tangu Puntland ilipoanza mashambulizi mwezi uliopita dhidi wanamgambo Daesh ambao wana mahandaki kwenye sehemu za milima za eneo hilo.

“Tumedhibitisha kuwa takriban wanamgambo 57 wa Daesh wote wakiwa raia wa kigeni waliuwawa kwenye mapigano katika saa 24 zilizopita,” Ahmed alisema. Hata hivyo Ahmed hakusema ni wanajeshi wangapi wa Puntland waliuwawa au kujeruhiwa ingawa aliashiria kuwa idadi ilikuwa kubwa.

Eneo la Puntland liomekuwa likishuhudia kwa muda sasa harakati za kundi la kigaidi la Daesh.