Wafanyabiashara watakiwa kutopandisha bei za bidhaa mwezi wa Ramadhan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i122474-wafanyabiashara_watakiwa_kutopandisha_bei_za_bidhaa_mwezi_wa_ramadhan
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza wafanyabiashara kujiandaa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kufanya biashara kwa uadilifu na kuwa na huruma kwa wananchi.
(last modified 2025-02-08T08:51:17+00:00 )
Feb 08, 2025 08:51 UTC
  • Wafanyabiashara watakiwa kutopandisha bei za bidhaa mwezi wa Ramadhan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza wafanyabiashara kujiandaa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kufanya biashara kwa uadilifu na kuwa na huruma kwa wananchi.

Alhaj Dkt. Mwinyi amesema, kumekuwa na kawaida na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bei bidhaa wakati huo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amefahamisha kuwa,  Serikali imekuwa ikipunguza ushuru katika Mwezi wa Ramadhani hivyo si jambo jema kwao kupandisha bei za bidhaa na kuwaongezea mzigo wananchi.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu ya Hijiria ambapo ndani yake Waislamu wamefaradhishiwa funga ya swaumu. Katika hadithi zimeelezwa fadhila mbalimbali za mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumzia suala la uchaguzi mkuu ujao Alhaj Dkt, Mwinyi amewasisitiza Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi Kudumisha Amani ili Uchaguzi huo Ufanyike kwa Utulivu na Amani.