Mjukuu wa Mandela: Hatutawaacha Wapalestina peke yao
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i130500-mjukuu_wa_mandela_hatutawaacha_wapalestina_peke_yao
Mjukuu wa kiongozi wa mapambano ya ukombozi wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela, Mandla Mandela amesisitiza kuwa, kamwe hatutawaacha peke yao Wapalestina huko Gaza na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel.
(last modified 2025-09-06T22:55:20+00:00 )
Sep 06, 2025 22:55 UTC
  • Mjukuu wa Mandela: Hatutawaacha Wapalestina peke yao

Mjukuu wa kiongozi wa mapambano ya ukombozi wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela, Mandla Mandela amesisitiza kuwa, kamwe hatutawaacha peke yao Wapalestina huko Gaza na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel.

Mwanaharakati huyo wa kimataifa amebainisha kwamba, muqawama wa kuwaunga mkono Wapalestina utaendelea hadi wapate uhuru wao.

Mjukuu wa Mandela amemebainisha hayo katika mkutano na waandishi wa habari nchini Tunisia akisisitiza kwa kusema: "Kamwe hatutawaacha peke yao Wapalestina huko Gaza na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu."

Mjukuu wa Nelson Mandela amesema: "Lazima tuhakikishe kuwa misaada ya kibinadamu inawafikia wanaostahili."

Ameongeza kuwa: "Kila mtu lazima atimize wajibu wake katika kueleza maafa ya Gaza. Ni lazima tutoe mashinikizo ili kuhakikisha kuwa suala la Palestina liko juu ya vipaumbele vya taasisi za kimataifa. Lazima tufanye kazi kupanua uungaji mkono kwa suala la Palestina katika ngazi ya serikali na nchi."

Mjukuu wa Nelson Mandela alisema: "Tunatumai kwamba meli za kusimama kidete kwa ajili ya kuvunja mzingiro wa Gaza vitasafiri kutoka Tunisia mnamo Septemba 7."

Mandla Mandela ameelekea Tunisia kujiunga na wanaharakati wengine wa kimataifa wanaoongoza msafara wa meli za misaada ya kibindamu kwa ajili ya watu wa Gaza wanaoendelea kufa kwa njaa ya kulazimishwaaan utawala wa Israel.

Makumi ya meli zinatarajiwa kuelekea Gaza kutoka Tunisia na bandari mbalimbali za Bahari ya Mediterania, na kujiunga na Global Sumud Flotilla.

Chama tawala nchini Afrika Kusini, African National Congress, kimeunga mkono ujumbe huo, kikisema "unaakisi mapambano yetu wenyewe kwa ajili ya ukombozi."