Jeshi la Mali lashambulia ngome za magaidi huko Kayes
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i130590-jeshi_la_mali_lashambulia_ngome_za_magaidi_huko_kayes
Jeshi la Mali limesema kuwa limefanya mashambulizi ya anga katika eneo la magharibi la Kayes lenye utajiri mkubwa wa dhahabu baada ya magaidi kuzuia kuingizwa mafuta katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bamako kutoka nje ya nchi hiyo.
(last modified 2025-09-09T03:31:28+00:00 )
Sep 09, 2025 03:31 UTC
  • Jeshi la Mali lashambulia ngome za magaidi huko Kayes

Jeshi la Mali limesema kuwa limefanya mashambulizi ya anga katika eneo la magharibi la Kayes lenye utajiri mkubwa wa dhahabu baada ya magaidi kuzuia kuingizwa mafuta katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bamako kutoka nje ya nchi hiyo.

Msemaji wa kundi moja ugaidi la huko Mali ametangaza kundi hilo limezuia kuingizwa mafuta nchini Mali kutoka nje ya nchi na kwamba wanatazamia pia kubana harakati za raia wa miji ya Kayes na Nioro, magharibi mwa Mali karibu na mpaka wa Senegal na Mauritania. 

Hadi sasa magaidi nchini Mali wamesimamisha malori barabarani katika mji wa Nioro na kupakua mafuta yote yaliyokuwe katika magari hayo. 

Akizungumza katika televisheni ya taifa, afisa wa jeshi la Mali ambaye jina lake halikutajwa amesema kuwa oparesheni zilizotekelezwa na jeshi hilo ni pamoja na mashambulizi ya anga dhidi ya magaidi na kwamba askari jeshi wamefanikiwa kuwakomboa raia waliokuwa wametekwa nyara na magaidi hao.  

Afisa wa muungano wa madereva wa malori nchini Mali amesema kuwa baadhi ya makampuni yamesitisha shughuli zake katika barabara inayoelekea Daka mji mkuu wa Senegal kutoka Bamako mji mkuu wa Mali.