HRW: Wanamgambo wamewaua zaidi ya watu 127 Niger
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i130650-hrw_wanamgambo_wamewaua_zaidi_ya_watu_127_niger
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, Wanamgambo wenye mfungamano na Kundi la kigaidi la Daesh wameua zaidi ya watu 127 nchini Niger.
(last modified 2025-09-10T23:44:03+00:00 )
Sep 10, 2025 23:44 UTC
  • HRW: Wanamgambo wamewaua zaidi ya watu 127 Niger

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, Wanamgambo wenye mfungamano na Kundi la kigaidi la Daesh wameua zaidi ya watu 127 nchini Niger.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa ripoti inayoonyesha kwamba kundi la wanamgambo wanaohusishwa na kundi la kigaidi la Daesh wamezidisha mashambulizi magharibi mwa nchi ya Niger na kuua zaidi ya watu 127 katika mashambulizi yao tofauti tangu mwezi Machi mwaka huu.

Ripoti hiyo iliangazia hali ya kiutu katika maeneo ya ukanda wa Sahel ambayo mara kwa mara yamekuwa yakikabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo ikiwemo katika mkoa wa Tillaberi, karibu na mpaka na Burkina Faso na Mali.

Ripoti hiyo iliangazia hali ya kiutu katika maeneo ya ukanda wa Sahel ambayo mara kwa mara yamekabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo ikiwemo katika mkoa wa Tillaberi, karibu na mpaka na Burkina Faso na Mali.

Eneo hilo la mpakani linajulikana kama kitovu cha shughuli za wanamgambo hao huko Afrika Magharibi na ambao pia wanatajwa kuwa na ushirikiano na makundi ya kigaidi Daesh na mtandao wa al-Qaeda.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kwamba mashuhuda wameeleza kuwa jeshi la Niger halijafanya vya kutosha kukabiliana na mashambulizi hayo na kupuuza maombi ya wanakijiji juu ya wasiwasi wao kiusalama. Niger haijatoa tamko lolote juu ya ripoti hiyo.