Wapinzani Zimbabwe: Haturudi nyuma, tutaendeleza maandamano dhidi ya Mugabe
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i13126-wapinzani_zimbabwe_haturudi_nyuma_tutaendeleza_maandamano_dhidi_ya_mugabe
Kiongozi wa wapinzani nchini Zimbabwe, Evan Mawarire amesema kuwa wataendeleza maandamano yao dhidi ya serikali ya Rais Robert Mugabe.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 12, 2016 10:35 UTC
  • Wapinzani Zimbabwe: Haturudi nyuma, tutaendeleza maandamano dhidi ya Mugabe

Kiongozi wa wapinzani nchini Zimbabwe, Evan Mawarire amesema kuwa wataendeleza maandamano yao dhidi ya serikali ya Rais Robert Mugabe.

Mawarire amesema kuwa maandamano dhidi ya serikali ya chama tawala cha ZANU-PF huko Harare, mji mkuu wa Zimbabwe, ya kulalamikia siasa mbovu na uchumi yatashadidi zaidi nchini. Amefafanua kuwa, kwa mshikamano wa Wazimbabwe kamwe hawatoridhia kuendelea hali mbaya kama ya sasa nchini na kwamba wameazimia kwa dhati kubadili hali hiyo. Wapinzani nchini Zimbabwe wanaamini kwamba baada ya ushindi wa chama tawala cha ZANU-PF katika uchaguzi mkuu miaka mitatu iliyopita, chama hicho hakijaweza kutekeleza ahadi zake hadi sasa.

Wazimbabwe wenye hasira mabarabarani

Malalamiko ya wapinzani juu ya hali mbaya ya uchumi na ukosefu wa ajira nchini Zimbabwe yanajiri katika hali ambayo chama tawala kinachoongozwa na Rais Mugabe, kilitumia mkono wa chuma katika kukabiliana na mikusanyiko yoyote ya hivi karibuni ya wapinzani nchini humo. Katika siku za hivi karibuni Zimbabwe ilishuhudia wimbi la maandamano ya wapinzani kufuatia kuongezeka mgogoro wa kiuchumi, kijamii na pia ukatili wa polisi dhidi ya raia.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe

Weledi wa mambo wanaamini kwamba, kuongezeka maandamano hayo ya raia ni hatari kubwa ya kijamii kwa serikali ya Rais Mugabe ambaye amekuwalo madarakani kwa kipindi kirefu.