Madagascar: Rais Rajoelina alaani jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i131596-madagascar_rais_rajoelina_alaani_jaribio_la_mapinduzi_dhidi_ya_serikali_yake
Rais Andry Rajoelina wa Madagascar ambaye serikali yake inakabiliwa na mashinikizo makuubwa ya maandamano amelaani kile alichokiita jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake.
(last modified 2025-10-04T22:57:00+00:00 )
Oct 04, 2025 22:57 UTC
  • Madagascar: Rais Rajoelina alaani jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake

Rais Andry Rajoelina wa Madagascar ambaye serikali yake inakabiliwa na mashinikizo makuubwa ya maandamano amelaani kile alichokiita jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake.

Katika video ya moja kwa moja iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii Andry Rajoelina alidai vijana waandamanaji 'wametumiwa kuchochea mapinduzi.

Kauli ya Rais Rajoelina inakuja kufuatia siku kadhaa za maandamano mabaya yanayoongozwa na vijana dhidi ya wasomi wa kisiasa na miaka mingi ya utawala mbaya.

Mikutano ya karibu kila siku ilianza Septemba 25 katika mji mkuu, Antananarivo, kuhusu uhaba wa umeme na maji na tangu wakati huo kuenea katika maeneo mengine ya kisiwa cha Bahari ya Hindi.

Waandamanaji wamemtaka rais ajiuzulu. Yakiitwa kuchukua hatua kwenye mitandao ya kijamii kupitia vuguvugu linaloitwa "Gen Z", maandamano hayo yalimlazimu Rajoelina kuifuta serikali yake na kukaribisha mazungumzo kurejesha utulivu.

Wametumiwa kuchochea mapinduzi, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 51 alisema akimaanisha waandamanaji ambao wengi wao ni vijana ambao wamejitokeza mitaani kuonyesha hasira zao. "Ninachotaka kukuambia ni kwamba baadhi ya watu wanataka kuharibu nchi yetu," alisema katika video ya moja kwa moja kwenye ukurasa wake wa Facebook, bila kutaja nani alikuwa nyuma ya hatua hiyo.

Umoja wa Mataifa umeripoti kuwa mgogoro wa Madagascar umesababisha vifo vya watu wasiopungua 22 na kujeruhiwa zaidi ya 100 katika kile kinachotajwa kama changamoto kubwa zaidi kuukabili utawala wa Rajoelina baada ya miaka kadhaa.