Samia amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Tanzania
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i133172-samia_amwapisha_mwigulu_nchemba_kuwa_waziri_mkuu_mpya_wa_tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amemwapisha Dk. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuthibitishwa na Bunge jana Alkhamisi Novemba 13, 2025.
(last modified 2025-11-14T12:20:52+00:00 )
Nov 14, 2025 11:12 UTC
  • Samia amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amemwapisha Dk. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuthibitishwa na Bunge jana Alkhamisi Novemba 13, 2025.

Rais Samia amesema wakati wa kumwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Tanzania kwamba uteuzi wake umepitia ushindani mkubwa.

Amesma licha ya kuwa na ushindani mkubwa lakini katika vigezo kadhaa, Dk Mwigulu amewashinda wenzake kwa sifa kidogo na kustahiki kuteuliwa kuchukua nafasi nzito wa Waziri Mkuu ambayo ni ya kusimamia wizara sote za serikali.

Hafla ya kumwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania imefanyika leo Ijumaa, Novemba 4, 2025. Hafla hiyo imefuatia hatua ya jana ya Rais Samia ya kumteua Nchemba kuwawaziri mkuu mpya na baadaye hiyo hiyo jana akapigiwa kura na kupitisha na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hafla ya kumwapisha Mwiguli imefanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozo waandamizi wa hivi sasa wa Serikali na wastaafu.

Moja ya vigezo vilivyotajwa na Rais Samia ni kwamba Mwigulu ametokea katika Wizara ya Fedha na anavijua vichochoro vyote ambavyo serikali ya Tanzania inapitia kukusanya fedha za maendeleo. Na kwa vile ahadi zilizotolewa na chama tawala CCM kwenye kampeni za uchaguzi zilikuwa ni nyingi na kubwa, zinahitaji fedha za kutosha. Hivyo amemtaka Waziri Mkuu mpya amsimamie vyema Waziri wa Fedha wa serikali ijayo ya Tanzania ili kufanikisha ilani ya uchaguzi ya CCM.