UN yalaani mauaji ya wakimbizi Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1501-un_yalaani_mauaji_ya_wakimbizi_sudan_kusini
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali mauaji ya yaliyotokea katika mojawapo ya vituo vya askari wa kulinda amani wa umoja huo huko Sudan Kusini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 19, 2016 00:08 UTC
  • UN yalaani mauaji ya wakimbizi Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali mauaji ya yaliyotokea katika mojawapo ya vituo vya askari wa kulinda amani wa umoja huo huko Sudan Kusini.

Ban Ki-moon amesema kuwa mapigano yaliyotokea baina ya makundi mawili hasimu katika kituo cha jumuiya hiyo ya kimataifa karibu na eneo la Malakal huko kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini yamesababisha mauaji ya watu wasiopungua 7 na kujeruhi wengine 40. Ban Ki-m Moon ameeleza wasiwasi wake kuhusu machafuko na mivutano inayoendelea baina ya makabila mawili ya Dinka na Shilluk na kutoa wito wa kujiepusha na matamshi au hatua yoyote inayoweza kuchochea machafuko zaidi. Amesisitzia kwamba mashambulizi yoyote dhidi ya raia, mafisa wa Umoja wa Mataifa na askari wa kulinda amani wa umoja huo yatatambuliwa kuwa ni jinai ya kivita.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka viongzo wa Sudan Kusini kutekeleza haraka makubaliano ya amani ili kuwawezesha raia wa nchi hiyo kuanza mchakato wa mapatano ya kitaifa.

Msemaji wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Ariane Quentier, jana alithibitisha kutokea hujuma hiyo ingawa hakutaja idadi ya waliouawa au kujeruhiwa.