Rais wa Senegal awaachilia huru mamia ya wafungwa kwa mnasaba wa Idi
Duru za habari nchini Senegal zimeripotia kuachiliwa huru mamia ya wafungwa kwa mnasaba wa sherehe za Idul-Adh'ha.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo karibu wafungwa 500 waliofungwa kwa makosa mbalimbali wameachiliwa huru leo kwa mnasaba wa siku ya Idi. Msamaha huo umetolewa na Rais Macky Sall wa nchi hiyo. Aidha duru za habari zimesisitiza kuwa, wafungwa wanaokabiliwa na tuhuma za mauaji na magendo ya madawa ya kulevya, hawakuhusishwa katika msamaha huo wa Rais Sall.
Kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul-Adh'ha, rais wa Senegal amesisitiza kufungamana na misingi ya kujali utu wa binaadamu na kutoa fursa kwa raia hata wasiokubaliana na sheria za nchi hiyo. Sikukuu ya Idul-Adh'ha imesherehekewa leo duniani kote.