Mwanaharakati: Saudia ilihusika kukandamizwa Waislamu Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1624-mwanaharakati_saudia_ilihusika_kukandamizwa_waislamu_nigeria
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imeukosoa utawala wa Aal-Saud kwa kutumia mamilioni ya dola kuishinikiza serikali ya Nigeria kuwakandamiza wafuasi wa harakati hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 20, 2016 12:09 UTC
  • Mwanaharakati: Saudia ilihusika kukandamizwa Waislamu Nigeria

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imeukosoa utawala wa Aal-Saud kwa kutumia mamilioni ya dola kuishinikiza serikali ya Nigeria kuwakandamiza wafuasi wa harakati hiyo.

Katika mahojiano na shirika la habari la Tasnim, Haroun Banawi, mwanachama wa harakati hiyo ya Kiislamu ya Nigeria amesema Saudi Arabia imetumia kiwango kikubwa cha pesa za mafuta kuihonga serikali ya Abuja ili ieneze fikra za Kiwahabi katika nchi hiyo ya Kiafrika sambamba na kuwakandamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia. Mwanaharakati huyo kadhalika amekosoa kile alichokitaja kuwa jinai na uhaini uliofanywa na jeshi la Nigeria katika mji wa Zaria Disemba mwaka uliopita wa 2015. Banawi amesema kuwa kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky anazuiliwa katika mazingira ya kutisha.

Itakumbukwa kuwa, tarehe 12 hadi 14 Disemba mwaka uliopita wa 2015, jeshi la Nigeria lilishambulia kituo cha kidini na nyumba ya kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky katika mji wa Zaria na kuua mamia ya Waislamu wasio na hatia. Hatima ya Sheikh Zakzaky ambaye alipigwa risasi kadhaa katika hujuma hiyo, bado haijajulikana mpaka sasa.