Waziri Mkuu wa Libya yupo tayari kufanya mazungumzo na Haftar
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i18061-waziri_mkuu_wa_libya_yupo_tayari_kufanya_mazungumzo_na_haftar
Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa na Baraza la Uongozi la Libya amesema yupo tayari kufanya mazungumzo na kamanda wa jeshi la taifa la nchi hiyo lililoko mashariki mwa nchi hiyo ili kutatua mgogoro wa Libya.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 24, 2016 09:48 UTC
  • Waziri Mkuu wa Libya yupo tayari kufanya mazungumzo na Haftar

Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa na Baraza la Uongozi la Libya amesema yupo tayari kufanya mazungumzo na kamanda wa jeshi la taifa la nchi hiyo lililoko mashariki mwa nchi hiyo ili kutatua mgogoro wa Libya.

Fayez al Siraj amesema kuwa, yupo tayari kukutana na kufanya mazungumzo na Jenerali Khalifa Haftar, kamanda wa jeshi la taifa la nchi hiyo na makamanda wengine wa jeshi ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Libya. Al Siraj ameashiria kuwa Khalifa al Ghawil, Spika wa Bunge lililovunjwa la Libya ameingia katika ikulu ya al Dhiyafa na anafanya jitihada za kuvuruga hali ya mambo na kuanzisha vita katika mji mkuu na kueleza kuwa, baadhi ya makundi ya kigaidi nchini humo yanatumia hitilafu za ndani na kunufaika na mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Libya.

Khalifa al Ghawil Spika wa bunge la Libya lililovunjwa

Mkuu wa Baraza la Uongozi la Libya amesema baadhi ya makundi yanafanya kila lialowezekana kuzusha mapigano ya umwagaji damu mjini Tripoli na kueleza kuwa, serikali yake inaamiliana na matukio mbalimbali  kwa hekima na busara na haitaki kutumia nguvu katika uwanja huo.

Itakumbukwa kuwa, serikali isiyo ya kisheria inayoongozwa na Khalifa al Ghawil tarehe 14 mwezi huu ilidhibiti ikulu ya al Dhiyafa ambayo ni makao makuu ya serikali mjini Tripoli.