Karenga Ramadhan ataka kulindwa waandishi habari Burundi
(last modified Wed, 26 Oct 2016 06:51:38 GMT )
Oct 26, 2016 06:51 UTC
  • Karenga Ramadhan ataka kulindwa waandishi habari  Burundi

Baraza la Taifa la Mawasiliano la Burundi limetaka kulindwa waandishi habari na kupewa uhuru zaidi utendaji kazi katika sekta hiyo.

Ramadhan Karenga Mkuu wa Baraza la Taifa la Mawasiliano la Burundi (CNC) amekosoa hali ya vyombo vya habari nchini humo na kueleza kuwa, suala la kuwalinda kimwili waandishi habari linapaswa  kujumuishwa katika sheria zinazohusiana na vyombo vya habari.  Waziri huyo wa Zamani wa Habari wa Burundi  amebainisha kuwa, ili kuweza kuwajibika vyema, waandishi habari wanahitaji kulindwa zaidi na kuwa na amani katika mazingira ya sasa ya hali mbaya ya mambo na kwamba kwa bahati mbaya baadhi ya waandishi habari hawastafidi na kadi zinazowatambulisha kuwa ni watu wa tasnia ya upashaji habari.  

Waandishi habari wa Burundi wakiandamana kudai kupatiwa uhuru katika tasnia yao

Ramadhan Karenga ameongeza kuwa sheria ya hivi karibuni inayohusiana na sekta ya vyombo vya habari ambayo ilipasishwa huko Burundi mwezi Mei mwaka jana imepingwa na aghalabu ya waandishi wa habari kwa sababu, sheria hiyo haikuzingatia haki zao ikiwemo haki ya kuwadhaminia usalama wao. Burundi inakabiliwa na mzozo wa ndani tangu mwezi Aprili mwaka jana baada ya Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo kusalia madarakani kinyume na katiba ya nchi. 

Tags