Mamia ya watoto waachiwa huru kutoka korokoro za serikali, Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i18358-mamia_ya_watoto_waachiwa_huru_kutoka_korokoro_za_serikali_nigeria
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa mamia ya watoto wameachiwa huru kutoka kwenye korokoro za serikali ya Nigeria.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Oct 29, 2016 04:47 UTC
  • Mamia ya watoto waachiwa huru kutoka korokoro za serikali, Nigeria

Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa mamia ya watoto wameachiwa huru kutoka kwenye korokoro za serikali ya Nigeria.

Mkurugenzi wa UNICEF katika masuala ya magharibi na katikati mwa Afrika, Manuel Fontaine, amesema kuwa, taasisi hiyo imefanikisha zoezi la kuachiwa huru watoto 876 waliokuwa wakishikiliwa katika korokoro za serikali ya Nigeria kwa kudhaniwa kuwa ni wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram.

Image Caption

 

Manuel Fontaine ameongeza kuwa, watoto hao walikuwa wakishikiliwa katika korokoro za mji wa Maiduguri na kwamba haijulikani wameshikiliwa huko kwa muda gani. Mkurugenzi wa UNICEF magharibi mwa Afrika amesema jeshi la Nigeria limekuwa likiwatia nguvuni na kuwafunga raia hususan watoto katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Boko Haram na kwamba suala hilo linapingwa vikali na jumuiya za kutetea haki za binadamu.

Hadi sasa jeshi la Nigeria halijatoa ufanunuzi kuhusu kadhia hiyo.