Maandamano yapigwa marufuku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i19774-maandamano_yapigwa_marufuku_jamhuri_ya_kidemokrasia_ya_kongo
Polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesisitiza kuwa ni marufuku kufanya maandamano katika miji mikubwa ya nchi hiyo ukiwemo mji mkuu Kinshasa, licha ya Umoja wa Mataifa kutaka kuheshimiwa uhuru na haki za msingi nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 19, 2016 04:36 UTC
  • Maandamano yapigwa marufuku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesisitiza kuwa ni marufuku kufanya maandamano katika miji mikubwa ya nchi hiyo ukiwemo mji mkuu Kinshasa, licha ya Umoja wa Mataifa kutaka kuheshimiwa uhuru na haki za msingi nchini humo.

Polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetahadharisha kuwa, itasambaratisha mkusanyiko wowote katika mji mkuu Kinshasa. 

Viongozi wa Kongo wamesema kuwa, hatua hiyo ya polisi ina lengo la kuzuia harakati za kuvuruga usalama katika jamii na kukaririwa machafuko kama yale yaliyouathiri mji wa Kinshasa siku kadhaa zilizopita. Polisi ya Kongo wamesema kuwa, watu wasiopungua 32 waliuawa kwenye ghasia za wapinzani zilitokea tarehe 19 na 20 mwezi Septemba mwaka huu. Hata hivyo chama cha upinzani cha Umoja kwa Ajili ya Demokrasia na Maendeleo ya Jamii (UDPS) kimeripoti kuwa watu 100 waliuliwa kwenye ghasia hizo.

Polisi ya Kongo imesema kuwa, itaimarisha usalama nchini humo hususan katika maeneo muhimu na ya kistratejia. Kambi ya wapinzani pia inasisitiza suala la kuzidisha mashinikizo kwa Rais Kabila katika mwezi mmoja uliosalia hadi kumalizika duru yake ya urais.

Rais Joseph Kabila wa Kongo ambaye alipasa kuondoka madarakani mwishoni mwaka huu kwa mujibu wa katiba

Kulingana na uamuzi uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kitaifa, uchaguzi wa Rais umepangwa kufanyika mwaka 2018. Wapinzani wanasema kuwa, Kabila kama walivyo baadhi ya viongozi wa nchi za Kiafrika, anadhamiria kung'ang'ania hatamu za uongozi hatua ambayo ni kinyume na katiba na misingi ya demokrasia.