Senegal yautaka Umoja wa Mataifa kulisaidia jeshi la kulinda amani la AU
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i19804-senegal_yautaka_umoja_wa_mataifa_kulisaidia_jeshi_la_kulinda_amani_la_au
Serikali ya Senegal imeutaka Umoja wa Mataifa kuusaidia kifedha Umoja wa Afrika katika kutekeleza majukumu na operesheni zake za kulinda amani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 20, 2016 04:05 UTC
  • Senegal yautaka Umoja wa Mataifa kulisaidia jeshi la kulinda amani la AU

Serikali ya Senegal imeutaka Umoja wa Mataifa kuusaidia kifedha Umoja wa Afrika katika kutekeleza majukumu na operesheni zake za kulinda amani.

Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Senegal, Mankeur Ndiaye ambaye alikuwa akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York amesema kuwa, kuna matatizo mengi yanayohusiana na kazi za askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika katika nchi za bara hilo na ametoa wito wa kutolewa misaada ya fedha na zana kwa majeshi ya Umoja wa Afrika na kushirikishwa zaidi Umoja wa Mataifa katika operesheni hiyo.

Askari wa Umoja wa Afrika nchini Somalia

Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Senegal amesema ni jambo la dharura kujadiliwa suala hilo na kushirikiana na Umoja wa Afrika kwa ajili ya kutatua matatizo yaliyopo katika uwanja huo.

Majeshi ya Umoja wa Afrika yanayolinda amani katika nchi mbalimbali za bara hilo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto nyingi hususan uhaba wa zana na bajeti ya shughuli za kusimamia amani katika nchi hizo.