Feb 27, 2016 16:50 UTC
  • Idadi ya wahanga wa homa ya manjano yapindukia 120 Angola

Idadi ya wahanga wa homa ya manjano (Yellow Fever) nchini Angola imeongezeka na kupindukia 120.

Maafisa wa afya wa Angola wametangaza kuwa, hadi sasa watu 125 wamepoteza maisha nchini humo kutokana na homa ya manjano. Eneo lililoathiriwa zaidi na homa hiyo ni mji mkuu, Luanda ambako watu wengi wamekumbwa ya ugonjwa huo usiotibika kirahisi.

Ripoti zinasema mgogoro wa bajeti umepelekea kukatwa fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kukusanya takataka nchini Angola na matokeo yake yamekuwa kurundikana uchafu na taka katika maeneo ya watu maskini kwenye jiji la Luanda.

Dalili za ugonjwa wa homa ya manjano ni pamoja na maumivu makali ya kichwa, kutapika na udhaifu wa mwili.

Maafisa wa sekta ya afya ya Angola wanasema kuwa, maradhi ya malaria na kipindupindu pia yameongezeka nchini humo.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa asilimia 90 ya vifo vinavyotokana na homa ya manjano vinatokea barani Afrika.

Tags