Wafanyabiashara Algeria wafanya mgomo wa nchi nzima
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22837-wafanyabiashara_algeria_wafanya_mgomo_wa_nchi_nzima
Wafanyabiashara nchini Algeria wameamua kufanya mgomo ikiwa ni hatua yao ya kulalamikia sheria mpya ya kodi.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Jan 04, 2017 12:36 UTC
  • Wafanyabiashara Algeria wafanya mgomo wa nchi nzima

Wafanyabiashara nchini Algeria wameamua kufanya mgomo ikiwa ni hatua yao ya kulalamikia sheria mpya ya kodi.

Wafanyabiashara katika miji mbalimbali ya Algeria wamefanya mgomo huo wa nchi nzima na kukabiliana na polisi ikiwa ni radiamali yao kwa sheria mpya ya nyongeza ya kodi iliyotangazwa hivi karibuni. Wafanyabiashara hao wanalalamikia sheria hiyo ya kodi ya mwaka mpya wa 2017 ambapo kodi imepandishwa kwa asilimia 30.

Wakati huo huo Nourddin  Bedoui, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Algeria pia ametoa radiamali yake kwa malalamiko hayo ya wafanya baishara wa nchi hiyo na kueleza kuwa, changamoto kuu inayoikabili Algeria katika mwaka mpya wa 2017 ni kuboresha ulinzi na usalama wa nchi hiyo. Amesema suala hilo ndio siasa ambazo zilitekelezwa pia mwaka jana wa 2016.

Wafanyabiashara wa Algeria wakikabiliana na polisi 

Waziri huyo ameongeza kuwa vitisho vya ugaidi na usalama vingali vinaendelea kuitatiza Algeria na kwamba serikali na jeshi zimejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa usalama wa nchi unalindwa kwa kila hali. 

Katika upande mwingine gazeti la al Watan la Algeria pia limetoa uchambuzi wake kuhusu suala hilo na kuandika, mgomo wa wafanyabiashara nchini humo unaendelea, hata hivyo bado haijafahamika ni shakhsia au ni jumuiya ipi iliyoagiza kufanyika mgomo huo.