Harakati ya Kiislamu Nigeria yalaani ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24191-harakati_ya_kiislamu_nigeria_yalaani_ukiukaji_wa_haki_za_binadamu_nchini_humo
Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria imelaani ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya nchi hiyo hususan haki za kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 24, 2017 11:28 UTC
  • Harakati ya Kiislamu Nigeria yalaani ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo

Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria imelaani ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya nchi hiyo hususan haki za kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky.

Taarifa iliyotolewa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetoa wito wa kuachiwa huru mara moja Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake na kusisitiza kuwa, kuendelea kumshikilia jela kiongoni huyo wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria ni ukiukaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa.

Wakati huo huo Waislamu wameendela kufanya maandamano katika maeneo mbalimbali ya Nigeria wakipinga hatua ya vyombo vya usalama kuendelea kumshikilia Sheikh Ibrahim Zakzaky licha ya uamuzi wa Mahakama Kuu iliyoarumu aachiwe huru bila ya masharti yoyote. 

Maandamano ya Waislamu nchini Nigeria

Mapema mwezi Disemba mwaka uliopita Jaji Gabriel Kolawole wa Mahakama Kuu ya Nigeria aliiamuru serikali na Nigeria kumwachilia huru bila ya masharti yoyote Sheikh Zakzaky na mke wake katika kipindi cha siku 45.    

Disemba mwaka juzi, jeshi la Nigeria lilishambulia msikiti na kituo cha kidini cha Baqiyatullah katika mji Zaria na kumtia mbaroni Sheikh Ibrahim Zakzaky, mkewe na makumi ya wanachama wa Harakati ya Kiislamu baada ya kuwauwa shahidi mamia ya wafuasi wa harakati hiyo waliokuwa kwenye shughuli ya kidini.