Umoja wa Afrika wasisitizia kuimarishwa demokrasia na utawala bora barani humo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24265-umoja_wa_afrika_wasisitizia_kuimarishwa_demokrasia_na_utawala_bora_barani_humo
Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bi, Nkosozana Dlamini Zuma ametaka kuimarishwa demokrasia na kuchungwa haki za binaadamu barani Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 26, 2017 04:09 UTC
  • Umoja wa Afrika wasisitizia kuimarishwa demokrasia na utawala bora barani humo

Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bi, Nkosozana Dlamini Zuma ametaka kuimarishwa demokrasia na kuchungwa haki za binaadamu barani Afrika.

Zuma ameyasema hayo katika hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia ambapo amesisitizia ulazima wa nchi wanachama kuzingatia matakwa ya wananchi, kuimarisha demokrasia, utawala bora na kuheshimu haki za binaadamu. 

Hali ya umasikini Afrika

Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amesema kuwa, katika hali ya sasa ya mabadiliko ya haraka duniai likiwemo ongezeko la tishio la ugaidi na mirengo ya kufurutu ada na ukatili, kukosekana uaminifu kati ya wanasiasa na raia na pia kukosekana usalama na uthabii, ni mambo yanayoliongezea changamoto kubwa bara la Afrika. Kwa ajili hiyo Bi, Dlamini Zuma ametaka kuharakishwa mwenendo wa kuanzishwa eneo huru la biashara na kupigwa hatua mabadilishano ya kibiashara baina ya nchi za Kiafrika kama ambavyo pia ametaka kuwepo uhuru katika sekta za usafirishaji wa bidhaa.

Uhaba wa chakula Afrika

Kikao hicho kilichofunguliwa Jumatano ya jana kinatazamiwa kuendelea kwa siku tatu ambapo Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 53 wanashiriki. Aidha kikao hicho kitajadili masuala kadhaa ikiwemo kadhia ya kuchaguliwa mkuu mpya wa kamisheni ya umoja wa Afrika atakayemrithi Bi, Dlamin Zuma.