Guterres: Nipo tayari kufanya juhudi za kurejesha amani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24471-guterres_nipo_tayari_kufanya_juhudi_za_kurejesha_amani_afrika
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, upo tayari kufanya juhudi za kurejesha amani katika nchi za Kiafrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 30, 2017 11:44 UTC
  • Guterres: Nipo tayari kufanya juhudi za kurejesha amani Afrika

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, upo tayari kufanya juhudi za kurejesha amani katika nchi za Kiafrika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa umoja huo upo tayari kufanya juhudi za kuona amani inapatikana barani Afrika. Guterres ameyasema hayo katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia.

Kikao cha 28 cha Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) huko Addis Ababa Ethiopia

Guterres ameashiria namna baadhi ya nchi za Kiafrika zilivyoshindwa kupiga hatua kubwa kiuchumi na kuongeza kuwa, umoja huo unafanya juhudi za kuanzisha mashirika kwa ajili ya ustawi endelevu katika nchi za Kiafrika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa hitilafu zilizopo kati ya nchi za Kiafrika zinaweza kupatia ufumbuzi kwa njia ya mazungumzo kwa kuungwa mkono na nchi wanachama wa umoja huo na ule wa kimataifa. Guterres amesema, atafanya jitihada zaidi za kutatua hitilafu na kuhitimisha mapigano barani Afrika. 

Mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika umeanza leo mjini Addis Ababa ukihudhuriwa na wawakilishi wa nchi 53 wanachama. Ajenda kuu ya mkutano huo ni kujadili masuala na matatizo ya nchi za Afrika.