Mazungumzo kati ya wapinzani na serikali yaahirishwa Kongo DR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24491-mazungumzo_kati_ya_wapinzani_na_serikali_yaahirishwa_kongo_dr
Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, limetangaza habari ya kuahirishwa mazungumzo baina ya serikali na wapinzani wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 31, 2017 01:03 UTC
  • Mazungumzo kati ya wapinzani na serikali yaahirishwa Kongo DR

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, limetangaza habari ya kuahirishwa mazungumzo baina ya serikali na wapinzani wa nchi hiyo.

Sambamba na kutangaza habari hiyo, Baraza hilop la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini humo limesema kuwa, sababu kuu iliyopelekea kuahirishwa mazungumzo hayo ni suala la uteuzi wa Waziri Mkuu. Hata hivyo baraza hilo limeongeza kuwa, mazungumzo bado yataendelea ingawa tarehe rasmi ya kuanza upya bado haijaainishwa. Wapinzani wa serikali wanataka uainishaji wa shakhsia mmoja kutoka upinzani ambaye atateuliwa kuwa Waziri Mkuu wa serikali.

Wapinzani wa kisiasa nchini Kongo DR

Hii ni katika hali ambayo kwa upande wake serikali inataka kuwasilishwa orodha ambayo kwa akali itakuwa na majina ya watu watatu kwa ajili ya uteuzi wa nafasi hiyo, kama ambavyo pia imetaka uteuzi huo ufanywe na Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo, suala ambalo limekataliwa na wapinzani. Tofauti nyingine baina ya serikali ya Kinshasa na wapinzani ni juu ya nafsi za uongozi wa wizara za sheria, fedha na masuala ya kigeni, suala ambalo kwa muda wote limekuwa na utata mkubwa katika mazungumzo hayo.

Mgogoro wa kisiasa nchini Kongo DR

Kwa mujibu wa makubaliano ya awali yaliyofikiwa tarehe 31 Disemba mwaka jana, rais Joseph Kabila licha ya kumalizika muhula wake wa uongozi, lakini ameruhusiwa kuendelea kuwa rais wa nchi hiyo hadi kutakapofanyika uchaguzi wa rais na bunge mwezi Disemba mwaka huu.