Feb 11, 2017 07:23 UTC
  • Watu 17 wafariki dunia katika msongamano kwenye uwanja wa mpira nchini Angola

Watu 17 wamefariki dunia na makumi ya wengine kujeruhiwa nchini Angola baada ya kutokea msongamano mkubwa katika uwanja mmoja wa mpira kaskazini mwa nchi hiyo.

Mkasa huo umetokea katika mji wa Uige katika mechi ya mpira wa miguu kati ya timu mbili za Santa Rita de Cassia na Recreativo do Libolo. 

Orlando Bernardo msemaji wa polisi ya Angola amdewaambia waandishi wa habari kwamba,  mkasa huo wa kusikitisha ulitokea jana katika mlango wa kaskazini wa kuingilia uwanjani ambapo watu 17 walipoteza maisha hapo hapo na wengine 56 kujeruhiwa kufuatia msongamano mkubwa uliojitokeza. 

Moja ya viwanja vya mpira nchini Angola

Miongoni mwa waliopoteza maisha wamo pia watoto kadhaa, imeeleza taarifa ya polisi ya Angola. Tukio hilo limetajwa kuwa ni maafa katika historia ya mchezo wa mpira wa miguu nchini Angola.

Rais  Jose Eduardo dos Santos ametuma salamu za pole na rambi rambirambi kwa familia zilizopoteza ndugu zao katika mkasa huo na ametoa agizo la kufanyika uchunguzi haraka iwezekanavyo ili kujua chanzo cha mkasa huo.

Tags