Wahajiri haramu raia wa Senegal, waliokuwa wanaelekea Ulaya, warejeshwa makwao
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25242-wahajiri_haramu_raia_wa_senegal_waliokuwa_wanaelekea_ulaya_warejeshwa_makwao
Wahajiri haramu 170 raia wa Senegal waliokuwa wamekusudia kuelea barani Ulaya na waliokuwa wamehifadhiwa katika kambi maalumu mjini Tripol, Libya wamerejeshwa makwao.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 17, 2017 04:05 UTC
  • Wahajiri haramu raia wa Senegal, waliokuwa wanaelekea Ulaya, warejeshwa makwao

Wahajiri haramu 170 raia wa Senegal waliokuwa wamekusudia kuelea barani Ulaya na waliokuwa wamehifadhiwa katika kambi maalumu mjini Tripol, Libya wamerejeshwa makwao.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, wahajiri hao walirejeshwa Alkhamisi ya jana katika fremu ya mpango wa kuwarejesha nyumbani wahajiri, mpango ambao unasimamiwa na Shirika la Kimataifa la Wahajiri (OIM). Kwa mujibu wa ripoti hiyo, karibu wahajiri wengine wapatao 200 raia wa Niger, walirejeshwa makwao siku ya Jumanne iliyopita kutoka Libya ambako baada ya kutiwa mbaroni, waliwekwa katika kambi maalumu nchini humo (Libya).

Ajali baharini zinazowakuta wahajiri hao

Mwaka jana Shirika la Kimataifa la Wahajiri (OIM) lilitangaza kuwa, liliwasaidia wahajiri 1589 kurejeshwa makwao kwa hiari wakati walipokuwa wakijaribu kuelekea barani Ulaya. Taarifa iliyotolewa mwezi Oktoba mwaka jana na OIM ilisema kuwa, zaidi ya wahajiri elfu tano walikuwa tayari wamefariki dunia tangu mwezi Aprili mwaka huo.

Wahajiri baada ya kuokolewa

Njia kuu ambayo mara nyingi hutumiwa na wahajiri hao kuelekea barani Ulaya wanakodhania kwamba wanaweza kupata maisha mazuri, ni Libya.