Waislamu Nigeria wawasilisha kilio chao kwa makamu wa rais ili kuwachiliwa Zakzaky
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25712-waislamu_nigeria_wawasilisha_kilio_chao_kwa_makamu_wa_rais_ili_kuwachiliwa_zakzaky
Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria imewasilisha kilio chake kwa makamu wa rais wa nchi hiyo ili kuachiliwa huru kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Yaqoub El Zakzaky.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 27, 2017 10:58 UTC
  • Waislamu Nigeria wawasilisha kilio chao kwa makamu wa rais ili kuwachiliwa Zakzaky

Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria imewasilisha kilio chake kwa makamu wa rais wa nchi hiyo ili kuachiliwa huru kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Yaqoub El Zakzaky.

Waislamu wa harakati hiyo sambamba na kufanya marasimu ya kuwakumbuka mashahidi wa mji wa Zaria, jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria, wamewasilisha kilio chao kwa Yemi Osinbajo, Makamu wa Rais wa nchi hiyo wakitaka kuachiliwa huru haraka iwezekanavyo kiongozi huyo wa kidini, mke pamoja na wanachama wengine wa harakati hiyo.

Sheikh Ibrahim Yaqoub El Zakzaky

Waislamu hao wamemtaka Osinbajo kuwaachilia huru shakhsia hao kwa mujibu wa amri ya mahakama kuu ya Federali ya mjini Abuja, iliyoiamuru serikali kumuachilia huru Sheikh Zakzaky. Akizungumzia barua ya malalamiko ya harakati hiyo kwa makamu huyo wa rais, Famy Fulana, wakili wa Sheikh Zakzaky amesema kuwa, kama ilivyopuuza amri ya mahakama kuu, serikali ya Nigeria imekiuka pia misingi ya sheria katika uwanja huo.

Yemi Osinbajo, Makamu wa Rais wa Nigeria

Amesema kuwa licha ya muhula uliotolewa na mahakama hiyo ya Federali kwa ajili ya kuachiliwa huru sheikh huyo kumalizika tarehe 16 Januari mwaka huu, lakini serikali hiyo haijatekeleza amri hiyo. Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa tarehe Pili Disemba mwaka jana na mahakama hiyo, kitendo cha kuendelea kushikiliwa na serikali ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Yaqoub El Zakzaky, mke na wanaharakati wengine wa Kishia ni kinyume cha sheria.