Makumi ya Wanigeria wafukuzwa Afrika Kusini, uhusiano wa nchi mbili matatani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25818-makumi_ya_wanigeria_wafukuzwa_afrika_kusini_uhusiano_wa_nchi_mbili_matatani
Msaidizi wa ngazi ya juu wa Rais wa Nigeria ametangaza kuwa, serikali ya Afrika Kusini imewafukuza raia 97 wa nchi hiyo kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa aina mbalimbali.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 02, 2017 00:05 UTC
  • Makumi ya Wanigeria wafukuzwa Afrika Kusini, uhusiano wa nchi mbili matatani

Msaidizi wa ngazi ya juu wa Rais wa Nigeria ametangaza kuwa, serikali ya Afrika Kusini imewafukuza raia 97 wa nchi hiyo kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa aina mbalimbali.

Hatua hiyo imechukuliwa wakati kukiwepo mivutano katika uhusiano wa Abuja na Pretoria kufuatia ghasia na machafujo ya wiki kadhaa nchini Afrika Kusini ambayo yanawalenga raia wa kigeni wanaoishi nchini huko hususan Wanigeria.

Msaidizi wa Rais wa Nigeria, Abike Dabiri-Erewa amesema Wanigeria waliofukuzwa Afrika Kusini wamewasili nyumbani na kwamba viza za kazi za wengi miongoni mwao zimefutwa.

Dabiri-Erewa ameongeza kuwa, Wanigeria hao walivamiwa kiholela na kwamba idadi ya Wanigeria wanaofukuzwa kutoka Afrika Kusini inatazamiwa kuongezeka katika siku zijazo.

Rais wa kigeni wanashambuliwa na kudhalilishwa Afrika Kusini

Wimbi la mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni lilipamba moto zaidi mwishoni mwa mwezi uliopita wa Februari nchini Afrika Kusini ambako wenyeji wanawatuhumu raia wa kigeni kuwa wamechukua nafasi zao za ajira na kuhusika na uhalifu unaotisha nchini humo. 

Mwezi uliopita pia Wanigeria walilipiza kisasi kwa kushambulia ofisi za kampuni ya simu ya Afrika Kusini ya MTN mjini Abuja  na baadhi yao wametoa wito wa kufukuzwa raia wa Afrika Kusini nchini kwao.