Takwa la kupambana na miamala haramu ya kifedha barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i3076-takwa_la_kupambana_na_miamala_haramu_ya_kifedha_barani_afrika
Rais Macky Sall wa Senegal ametoa wito wa kuanzishw amapambano dhidi ya miamala haramu ya kifedha barani Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 14, 2016 23:32 UTC
  • Takwa la kupambana na miamala haramu ya kifedha barani Afrika

Rais Macky Sall wa Senegal ametoa wito wa kuanzishw amapambano dhidi ya miamala haramu ya kifedha barani Afrika.

Rais wa Senegal ametoa wito huo katika mkutano wa kiuchumi uliofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Dakar ukihudhuriwa na wataalamu 40, wakuu wa makampuni mbalimbali na viongozi wa jumuiya za kimataifa. Macky Sall amesema kuwa, juhudi za kuzuia na kupambana na miamala haramu ya kifedha barani Afrika zinahitaji ushirikiano wa kimataifa na kwamba tatizo hilo linasababisha hasara ya dola baina ya bilioni 50 hadi 148 kwa mwaka kwa nchi za Kiafrika.

Rais Macky Sall wa Senegal ameongeza kuwa rasilimali za Afrika zinaporwa na kwamba nchi za Kiafrika zinapaswa kushiikiana na washirika wao kwa ajili ya kulinda rasilimali na utajiri wa bara hilo. Vilevilke amewataka wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusaidia mchakato wa kubuni sheria mpya kwa ajili ya nchi za Afrika.

Amesema makampuni mbalimbali yanapaswa kulipa kwanza ushuru wao katika nchi zinakozalisha maliasili tajiri.

Matamshi hayo ya Rais wa Senegal wakati bara la Afrika lenye utajiri wa maliasili wa madini, mazingira asilia na maeneo muhimu ya kijigrafia, jamii vijana na uwezo mkubwa wa kustawi kiuchumi likikabiliwa na changamoto nyingi. Viongozi wengi wa nchi za Kiafrika pia wamekumbwa na maradhi ya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma. Vilevile kuwepo kwa magenge ya magendo za aina mbalimbali, makundi ya kigaidi na vita na mapigano ya ndani ya kikabila la kikaumu vimezidi kuwafanya wakazi wengi wa Afrika waendele kuishi katika ukata uliopindukia. Wakati hui hui ustawi wa kiuchumi katika nchi nyingi za Kiafrika bado ni wa kiwango cha chini na kiwango kikubwa cha fedha za haramu kitanoa pigo kwa uchumi wa nchi za bara hilo.

Katika upande mwingine ushawishi wa nchi za kikoloni barani Afrika unaoendelezwa chini ya mwavuli wa kutekeleza miradi ya kiuchumi na uwekezaji na vilevile uchimbaji wa madini tajiri havisaidi kuboresha uchumi wa Afrika. Nchi hizo pia hazipati maslahi yoyote kutokana na shughuli hizo kutokana na kutolipwa kodi na kutoheshimiwa sheria za ndani ya nchi. Vilevile unyonyaji wa nguvu kazi na kutumiwa malighafi za bei nafuu umekuwa na faida kwa nchi za kikoloni badala ya kuwanufaishi watu wa nchi za Afrika.

Siku chache zilizopita Shirika la Uwazi la Kimataifa (Transparency International) lilitoa ripoti likizungumzia ongezeko kubwa la ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma barani Afrika. Baadhi ya nchi zilizoashiriwa katika ripoti hiyo ni Afrika Kusini, Ghana na Nigeria. Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo, uchunguzi uliofanyika katika nchi 28 umeonesha kuwa, polisi, wakurugenzi wa masuala ya kibiashara, maafisa wa serikali na mahakama ni miongoni mwa watu na taasisi zilizozama katika ufisadi.

Ripoti ya Transparency International pia imeonesha kwamba gharama za kununua silaha zimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni kwenye nchi za Kiafrika kwa ajili ya kupambana na makundi ya kigaidi huko kaskazini, magharibi na katika Pembe ya Afrika. Kituo cha uchunguzi wa amani cha Stockholm International Peace Research Institute kimeripoti kuwa, bajeti ya masuala ya kijeshi ya nchi za Kiafrika imeongezeka kwa asilimia 91 katika kipindi cha muongo mmoja uliopita a kufikia dola bilioni 40 mwaka 2015. Kimesema kwua hii ni katika hali ambayo hakuna usimamizi kamili wa mikataba ya silaha, suala ambalo limesabisha ufisadi katika miamala hiyo.

Kutokana na haya yote baadhi ya viongozi wa nchi za Kiafrika wanaonekana kuchoshwa hali ya sasa na wanatafuta njia kutatua tatizo hilo. matamshi ya Rais Macky Sall wa Senegal yanatathminiwa katika mkondo huo.