Morocco: Afrika ichukue hatua shirikishi kukabiliana na wimbi la uhajiri
(last modified Tue, 04 Jul 2017 07:47:57 GMT )
Jul 04, 2017 07:47 UTC
  • Morocco: Afrika ichukue hatua shirikishi kukabiliana na wimbi la uhajiri

Mfalme Mohammed VI wa Morocco imetoa mwito kuzitaka nchi za Afrika kuchukua hatua ya pamoja kwa ajili ya kukabiliana na wimbi la uhajiri.

Mfalme Mohammed VI ameyasema hayo katika hotuba iliyorushwa na vyombo vya habari vya serikali na kusema kuwa, kufuatia ongezeko la wimbi la uhajiri, Rabat itawasilisha penekezo la kuchukuliwa hatua shirikishi juu ya kupambana na tatizo hilo kwa nchi za Kiafrika. Kwa mujibu wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco, maelfu ya vijana wa Kiafrika na katika kujaribu kutafuta maisha bora huhajiri kupitia njia zisizo halali kwa kuvuka bahari ya Mediterranean wakielekea Ulaya.

Wahajiri wakiwa ndani ya boti wakijaribu kuvuka bahari

Katika jitihada hizo za wahajiri, aghlabu yao hupoteza maisha kwa kuzama maji baharini au kwa kukosa maji na njaa kali jangwani, kabla ya kufika maeneo wanayoelekea. Kadhalika Mfalme Mohammed VI amewataka viongozi wa Kiafrika kukubali majukumu yao katika kukabiliana na suala hilo ambalo limegeuka na kuwa changamoto kubwa kwa mataifa mbalimbali ya Ulaya na Afrika. Kwa mujibu wa Shirika la Wahajiri Duniani IOM, watu wanaofanya biashara haramu ya magendo ya wahajiri wanatengeneza faida ya dola bilioni 35 za Marekani kwa mwaka pasina kujali namna wanavyohatarisha maisha ya maelfu ya wahajiri. 

Miili ya wahajiri waliofia baharini ikiopolewa

Mwaka uliopita pekee, wahajiri zaidi ya elfu tano aghlabau wakiwa raia wa nchi za Nigeria, Eritrea, Somalia, Sudan, Gambia, Senegal, Mali, Morocco na Tunisia Aghalabu walifariki dunia kwa kuzama katika bahari ya Medittaraenia wakiwa katika safari hizo hatari za kuelekea Ulaya, kwenda kutafuta kazi na maisha mazuri.

Tags