Eneo muhimu ya Kipese DRC lakombolewa na jeshi kutoka mikoni mwa waasi
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limetangaza kuwa, eneo la kiistratejia la Kipese lililokuwa chini ya udhibiti wa wanamgambo wanaobeba silaha limekombolewa la jeshi la nchi hiyo.
Msemaji wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mkoa wa Kivu Kaskazini alisema jana Jumapili kwamba, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kulikomboa eneo la Kipese lililokuwa likidhibitiwa na kundi la wanamgambo wa Mai-Mai.
Kwa mujibu wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni kuwa, wanajeshi wawili na wanamgambo watano wa Mai-Mai wameuawa katika mapigano ya klikomboa eneo eneo.
Ripoti zinasema kuwa, jeshi la DRC sasa limeanzisha operesheni kali ya kulisafisha eneo hilo na uwepo wa wanachama wa kundi la wanamgambo wa Mai-Mai.
Maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamekuwa yakishuhudia machafuko na mapigano kwa miaka kadhaa sasa kutokana na ngome ya makundi ya waasi.
Hayo yanajiri huku eneo la katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekuwa likishuhudia machafuko ya umwagaji damu tangu mwezi Septemba 2016 na tangu wakati huo hadi hivi sasa, vikosi vya serikali vinapambana na kundi moja la waasi lililozuka kwenye eneo hilo.
Ukosefu wa amani na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliifanya Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo CENI itangaze kwamba, uchaguzi wa Rais hauwezi kufanyika mwaka huu. Hata hivyo tangazo hilo limetafsiriwa na wapinzani kwamba, ni njama za kutaka kumuandalia mazingira Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo aendelee kubakia madarakani.