Mali yathibitisha kutiwa mbaroni gaidi wa harakati ya Macina
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i32176-mali_yathibitisha_kutiwa_mbaroni_gaidi_wa_harakati_ya_macina
Wanajeshi wa Mali na Ufaransa wamemtia mbaroni mshirika wa karibu wa mhubiri wa huko Mali ambaye kundi lake lenye misimamo mikali limedai kuhusika na makumi ya mashambulizi dhidi ya maslahi ya magharibi na Mali. Hayo yameelezwa na Waziri wa Usalama wa Mali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 23, 2017 23:25 UTC
  • Mali yathibitisha kutiwa mbaroni gaidi wa harakati ya Macina

Wanajeshi wa Mali na Ufaransa wamemtia mbaroni mshirika wa karibu wa mhubiri wa huko Mali ambaye kundi lake lenye misimamo mikali limedai kuhusika na makumi ya mashambulizi dhidi ya maslahi ya magharibi na Mali. Hayo yameelezwa na Waziri wa Usalama wa Mali.

Harakati ya Ukombozi ya Macina yenye makao yake katika mkoa wa Mopti katikati mwa Mali inaongozwa na mhubiri Amadou Koufa ambaye amewatolea wito wafausi wake kubeba silaha na kuhuisha ufalme wa kihistoria wa Fulani huko Massina. Jenerali Salif Traore amesema amethibitisha kuwa gaidi Alhousseyn Asssaleh ambaye ni mkuu wa masuala ya kilojistiki wa harakati ya Ukombozi ya Macina inayoongozwa na Amadou Koufa alikamatwa tarehe 8 mwezi huu katika oparesheni ya pamoja ya kikosi cha kupambana na ugaidi kwa jina la Barkhane huko Timbuktu.

Kikosi cha pamoja cha kupambana na ugaidi kikiwa kaskazini mwa Mali 

Waziri wa Ulinzi wa Mali ameongeza kuwa kutiwa mbaroni kwa gaidi huyo kulikuwa kumefanywa siri hadi sasa kwa sababu ya jitihada zinazoendelea za kuwatia mbaroni magaidi wengine katika mtandao huo.